Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewasifu wabunge wa upinzani, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) ambaye ni mbunge wa Vunjo na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), Mbunge wa Kigoma mjini kwa kutoa hoja nzito huku akiwaponda baadhi ya wabunge wa upinzani.

Lukuvi alitoa sifa hizo leo wakati akichangia katika kikao cha bunge. Alieleza kuwa wabunge hao wa upinzani wamekuwa wakitoa hoja nzito bila kutumia lugha zenye ukakasi na kuwashambulia mawaziri kama wanavyofanya wabunge wengine.

“Kuna wabunge wa upinzani kama Mbatia… Zitto, wanatoa hoja nzito sana bila kutumia lugha za matusi. Lakini hoja zao ni nzito,” alisema Lukuvi.

Waziri huyo alionesha kukerwa na baadhi ya wabunge wa upinzani ambao amedai wamekuwa wakiwashambulia mawaziri bila kufikiria kuwa na wao ni wabunge kama wao. Alisema wabunge hao wanapotoa hoja zao bungeni huwaita mawaziri ‘wajinga’, ‘wapumbavu’ na lugha nyingine zisifaaa, kitendo ambacho amekilaani.

Mbunge wa Upinzani atimuliwa bungeni
Mbeya City Waibanjua JKT Ruvu