PRISONS leo imeshinda bao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku mashabiki wao wakibeba bango lenye ujumbe uliosomeka hivi ‘Wao Basi, sisi soka’ ikiwa na maana kwamba Mbeya City wamenunua basi wao wanacheza soka.

Ujumbe huo unatokana na mwenendo mbovu wa City huku leo wakipigwa bao 4-1 na Ndanda Fc, mechi hiyo imechezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Azam yenye imerudi kileleni kwa kufikisha pointi 39 na kuishusha Yanga ambayo ina pointi 36 na inacheza kesho Alhamisi. Azam wamepanda kileleni baada ya kuifunga Mgambo JKT bao 2-1, mechi iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mabao ya Prisons yalifungwa na Jeremiah Juma dakika ya 61 baada ya kupiga shuti kali na kutinga nyavuni ikiwa ni piga nikupige langoni mwa wapinzani wao wakati bao la pili lilifungwa na Mohamed Mkopi dakika ya 82.

Mkopi alifunga bao hilo baada ya kupokea krosi ya Benjamini Asukile huku bao la kufutia machozi la Coastal Union likifungwa na Mtenje Juma dakika ya 76 akiunganisha krosi ya Amad Juma.

Katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Stand United imefanikiwa kubaki na pointi tatu baada ya kuifunga Toto Africans ya jijini Mwanza bao 2-1.

Ndanda FC Watakata Nyumbani
Jukwaa la Wahariri Lamkosoa Nape, mawio lapata mtetezi