Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dk John Magufuli ameendelea kuwasisitiza makandarasi wazembe kujianza kujiondoa taratibu katika nafasi walizopo kwakuwa hatawavumilia atakapoingia madarakani.

Dk Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, ameweka msisitizo huo jana wakati akifunga mkutano wa wahandisi.

Alisema kuwa serikali yake itawapa wahandisi mishahara mikubwa lakini pia itawataka wafanye kazi kubwa inayoendana na mshahara wanaopokea.

Aliongeza kuwa wakandarasi na wahandisi wanaofanya kazi zao vizuri hana tatizo nao lakini hatawavumilia htta kidogo wale ambao wanatia doa taaluma hiyo.

“Wahandisi nawafahamu vizuri kwa kuwa nimefanya kazi nanyi na ninaahidi nitakuwa nanyi bega kwa bega kuhakikisha taaluma hii inazidi kukua na kuheshimika,” alieleza.

 

 

Wananchi Waibadilikia CCM
Lowassa: CCM Wamekumbuka Shuka Kumekucha