Moja kati ya mambo ambayo mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walivutiwa nayo kwenye video kubwa ya wimbo wa Diamond aliyoipa jina la ‘Utanipenda’, ni uhalisia wa mazingira na uwepo wa mama yake mzazi na mwanaye Tiffah.

Hata hivyo, mama mzazi wa Diamond ameeleza kuwa alipata shida na maumivu wakati anaigiza kuwa ameenda kuomba msaada kwa Said Fella na rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika kipindi maalum kinachoelezea utengenezaji wa video hiyo, mama Diamond alisema kuwa alipata changamoto kubwa ya maumivu wakati anajaribu kupiga magoti kwa sababu alikuwa bado hajapona vizuri kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamkabili.

Alisema kuwa wakati anainama kupiga magoti, alisikia miguu maumivi kwenye magoti lakini ilibidi afanye zoezi hilo mara kadhaa ili kupata scene nzuri kwa kuwa Said Fella alionekana kumuonea huruma kweli hali iliyowafanya kurudia mara kadhaa.

Kwa upande wa Diamond, alieleza kuwa alijisikia maumivu pia moyoni alipokuwa akimuona mama yake na mtoto wake (Tiffah) mgongoni kwake wakiomba msaada. Alipojaribu kuvuta taswira ya kweli, alishindwa kuangalia.

“Kuna wakati nilikuwa nikiangalia ninamuona mama kweli anapiga magoti wanamfukuza… na mtoto wangu, nilijisikia vibaya na nikawa naenda mbali nisiangalie kabisa kwa sababu nilikuwa navuta taswira kama kweli,” alisema Diamond.

Msanii huyu wa Bongo Movie aamua kumpa Figo mama yake
Nisher azungumzia Mpango wa Kuokoka, ajibu tuhuma za kutumia fedha za baba kuchapia

Comments

comments