Moyo wa upendo hupimwa katika wakati mgumu, na upendo wa mama aliyekutunza tumboni kwake na kukupa maisha hauwezi kurudishwa ila unaweza kuonesha namna unavyojali kwa kiwango fulani.

Hali hiyo imempelekea msanii wa Bongo Movies, Sabrina Omary maarufu kama Sabby aliyeonekana zaidi kupitia filamu ya Riziki, kuamua kumpa figo mama yake ambaye anasumbuliwa na tatizo la figo na madaktari wamependekeza awekewe figo ya mtu mwingine yenye afya bora zaidi.

Sabby

Sabby

Akizungumza nwa mwandishi wa Globalpublishers, Sabby ameeleza kuwa ameamua kusitisha masomo yake nchini Marekani ili aweze kumpa mama yake huyo figo.

“Tatizo la figo kwa mama yangu ni la muda mrefu na limekuwa likinikosesha raha mno. Kwa sasa nimejitoa kama wakiniambia inahitajika mtu atoe figo niko tayari kumpatia,” Sabby anakaririwa.

'Msanii mwenye bifu na Diamond hawezi kutoboa kimataifa'
Mama yake Diamond Alipata maumivu alipokuwa anashuti 'Utanipenda'