Mwanaharakati na muasisi wa harakati ya Change Tanzania, Maria Sarungi ameonesha kushangazwa na taarifa za Chadema alizodai zimemtaja kuwa alinunuliwa na CCM kusaidia kufikisha matokeo ya utafiti wa Twaweza uliompa ushindi Mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli kwa asilimia 65 dhidi ya Edward Lowassa wa Chadema.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Maria Sarungi ambaye hivi sasa amekuwa akikutana na changamoto kubwa ya jumbe zinazomkosoa zinazoaminika kuwa zinatoka kwa watu wanaounga mkono Ukawa, alisikitishwa na jinsi ambavyo akaunti inayoaminika kuwa rasmi ya Chadema ilivyodai amenunuliwa.

Angalia Orodha Ya Mawakala Wenye Mkwanja Mrefu
Zico Alia Na Kanuni Za Uchaguzi FIFA