Saa chache kabla ya kuelekea kwenye pambano wa Mzunguuko wa nane wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mabingwa Watetezi Simba SC, Afisa Habari wa Maafande wa Ruvu Shooting Masau Bwire amechimba mkwara mzito.

Masau ambaye anasifika kuwa na maneno ya shombo dhidi ya timu pinzani, amesema wana imani kubwa leo Jumatatu Oktoba 26 wanakwenda kuibamiza Simba SC ambayo ilipoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons.

Amesema ili wapinznai wao wasiwe na kisingizio, amewataka kupanga kikosi chao kamili tofauti na ilivyokua dhidi ya Tanzania Prisons, ambapo baadhi ya wachezaji walikosekana, na kuchukuliwa kama sababu ya kuangusha alama tatu mjini Sumbawanga, Rukwa.

“Tunawataka Simba leo wapange kikosi kamili, ili wasiwe na kisingizio tukiwafunga.. Wao wanasema wana mpira kachori, kachori kitu gani bwana !! Watakutana na mpira KAUKAU”. Amesema Masau Bwire

Katika mchezo huo Ruvu Shooting watakua wageni wa Simba SC, huku wakiwa na kumbukumbu ya kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Kinondoni Municipal Council (KMC FC) katika mchezo uliopita.

Simba SC inayonolewa na kocha SVEN Vandenbroeck ipo nafasi ya tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu kwa kufikasha alama 13, huku wageni wao Ruvu Shooting wakishika nafasi ya 11 kwa kuwa na alama 9.

Kadinali wa kwanza apatikana Rwanda
Sure Boy, Chirwa kuikosa Mtibwa Sugar

Comments

comments