Mmoja kati ya watunga sheria nchini Urusi aliyetajwa kwa jina la Oksana Bobrovsk mwenye umri wa miaka 30 amekufa katika mlipuko uliotokea kwenye gari walilokuwa na mumewe, huku miili yao ikikutwa nusu watupu.

Miili hiyo ilikutwa kwenye gari hilo aina ya Toyota RAV-4 nyuma ya kiti cha abiria ambapo taarifa zilidai kuwa wawili hao walikuwa wakijaribu kufanya mapenzi kabla ya mlipuko huo kutokea.

Oksana Bobrovskaya akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao wa kike

Oksana Bobrovskaya akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao wa kike

Taarifa zilizoripotiwa na mtandao wa Siberian Times zinaeleza kuwa mashuhuda wamesema kuwa mume wa Oksana aliyetajwa kwa jina la Nikita Tislenko mwenye umri wa miaka 28 alikuwa anahisi kuwa anamsaliti kwa kutoka na mfanyabiashara mmoja mkubwa na kwamba alipanga kumfanyia tukio.

Imeelezwa kuwa wakiwa ndani ya gari, Nikita alijaribu kufanya mapenzi na Oksana na baada ya kutokea sintofahamu alifyatua kilipuzi alichokuwa nacho kwenye gari hilo na kusababisha wote wawili kupoteza maisha.

Mwanaume huyo anatajwa kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi wa jeshi la Urusi.

Mkuu wa kitengo cha upelelezi cha wilaya ya Oktyabrsky, Vitaly Latypov aliiambia Siberian Times kuwa ‘guruneti’ lilitumika katika mlipuko huo. Hata hivyo,

Jeshi la Politi katika jimbo la Novosibirsk analoliwakilisha mwanamke huyo lilisema kuwa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo itatoka baada ya uchunguzi kukamilika.

Messi amfunika Ronaldo Tuzo za La Liga
Makontena Tisa Yakamatwa Dar