Baada ya Waziri wa ardhi, William Lukuvi kutangaza kuwa eneo la ekari 1500 lililopo Lingato Kisarawe 11, Kigamboni Dar es salaam alilopewa Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda kwa ajili ya ujenzi viwanda vidogo vidogo kuwa ni eneo la Serikali, mmiliki wa eneo hilo mfanyabiashara Mohamed Iqbal ametoa vielelezo vya umiliki wa eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 3, 2017,  Kamugisha Katabara ambaye ni mwakilishi wa Mohamed Iqbar katika ukumbi ya jengo la Red Cross jijini Dar es salaam amesema kuwa ushahidi wa nakala za barua za mawasiliano kati ya ofisi ya serikali ya mtaa wa Lingato,muhtasari ya vikao vya maamuzi ya serikali za mitaa na mikutano na wananchi waliomiliki maeneo hayo ipo.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi mnamo tarehe 27, Februari mwaka huu imeeleza kuwa “eneo hilo siyo la mfanyabiashara huyo ni mali ya Serikali, hivyo mfanyabiashara huyo amemdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kumpatia eneo ambalo si mali yake bali ni mali ya Serikali, kufuatia kushindwa kesi kati yake na wananchi.”

Kamugisha amesema kuwa tuhuma hizo zimewasikitisha wataalamu wanaotambua jambo hilo kumuondolea heshima ndugu Iqbal, hivyo wameamua kuwaita waandishi wa habari ili kufikisha ukweli kwa umma juu ya mambo haya matatu ikiwa ni pamoja na umiliki wa eneo, utaratibu wa kukabidhi eneo kwa mkuu wa mkoa huyo, na hukumu ya kesi aliyoizungumzia Waziri wa ardhi.

Amesema Ndugu Iqbal ni mmiliki halali wa eneo hilo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 3500, amesema alinunua eneo hilo tangu mwaka 2005 kutoka kwa wananchi wa eneo hilo ambao waliuza kwa hiari yao wenyewe bila kushurutishwa na kwa kufuata taratibu zote za kisheria za ununuzi wa ardhi.

Aidha Kamugisha ametoa uhalali wa umiliki wa eneo hilo huku akisema kuwa endapo zitahitajika zitawekwa bayana nakala pamoja na picha.

“Ushahidi wa nakala za barua za mawasiliano kati ya ofisi ya serikali ya mtaa wa Lingato,muhtasari ya vikao vya maamuzi ya serikali za mitaa na mikutano na wananchi waliomiliki maeneo hayo ipo. Aidha nakala za risiti zipo na malipo ya ushuru wa serikali kama sheria inavyotaka na mikataba ya mauziano ya maeneo ya ardhi na picha za wamiliki wa maeneo wakipokea fedha za malipo na mauziano ya ardhi zipo na zitawekwa bayana pale zitakapohitajika.” amesema Kamugisha

Mbunge asusia kikao cha madiwani
Watuhumiwa 11,303 dawa za kulevya wakamatwa