Djumbe Joseph aliyepitishwa na (NEC) kugombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, ameandika barua ya kujitoa katika uchaguzi mdogo ambao unatarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 kwa kile alichosema anafuata msimamo wa chama chake.

Akiongea na waandishi wa habari Djumbe Joseph amesema kuwa ameamua kuungana na viongozi wakuu wa chama chake kutoshiriki katika uchaguzi huo mdogo ambao unategemewa kufanyika mapema Januari 2018.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kilitangaza kuwa hakiweka muakilishi yoyote kugombea jimbo hilo la Singida Kaskazini kwa kile walichosema awali kuwa hawawezi kushiriki uchaguzi huo wa marudio bila tathimini kufanyika juu ya uchaguzi wa udiwani uliofanyika karibuni ambao ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki na sheria pamoja na watu kupigwa hovyo.

 

Mwenyekiti NCCR-Mageuzi apata ajali mbaya
Video: Wanaosema vyuma vimekaza washughulikiwe- JPM