Mgombea Ubunge wa Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma kupitia NCCR-Mageuzi, Ugin Mkinga ametangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hiyo .

Akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa amefikia uamuzi huo ili aongeze nguvu kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM), kwani mambo anayoyataka ndiyo ambayo Rais Dkt. Magufuli anafanya.

“Sababu ya kujitoa ni kuridhishwa na uongozi wa Dkt,John Pombe Magufuli.Kama CCM watajiskia niamie kwao nipo tayari wakati wowote na nitamuunga mkono Mbunge wangu ambaye yupo kwa kipindi hiki,”Amesema Mkinga.

Mkinga ameeleza kuwa vyama vya upinzani havijawa tayari kuongoza na kuchukua dola na muda wowote yuko tayari kuungana na CCM.

“Nimeamua kujitoa rasmi katika kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge jimbo la Madaba mkoa wa Ruvuma kwasababu moja, udhaifu wa mfumo wa vyama vya upinzani kwa sababu havina taswira ya kuchukua Dola,” amesema Mkinga.

Dkt. Bashiru aongoza waombolezaji mazishi ya watoto Kagera
Washitakiwa Kifo cha Dokta Mvungi wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Comments

comments