Waziri wa Nishati, January Makamba amesema milango ya Tanzania ipo wazi kwenye uwekezaji wa sekta ya Nishati, kutokana na uwepo wa mahitaji makubwa ya Nishati katika uzalishaji na Usambazaji kwenye maeneo ya sekta hiyo.
Waziri Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa sekta ya Nishati, Wawekezaji, Makampuni ya Nishati kutoka Nje, Mabalozi wa Nchi mbalimbali ambao unaangazia hali ya sekta ya Nishati sambamba na maendeleo yaliyofikiwa, Mkutano ulioandaliwa na Energy Net Afrika.
Amesema, “Kwanini Tanzania, Kwanini sasa? Tanzania ni mahali sahihi penye amani katika kufanya uwekezaji, hivyo tunawakaribisha Wawekezaji wenye tija kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati Nchini.”
Kwa upande wao Washiriki katika Mkutano huo wamepongeza juhudi za Serikali katika Sekta ya Nishati kwa kufungua wigo wa Uwekezaji sambamba na kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo urasimu.