Milionea aliyetajwa kwa jina la Devinder Kainth (pichani) ambaye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua mtu aliyempiga picha mwanae wa kike akiamini alivutiwa nae kimapenzi, amesamehewa kwenda jela.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, milionea huyo alikuwa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukiri kuwa alimuua bila kukusudia Sandro Rottman kwenye mgahawa mmoja maarufu nchini Hispania.

Hata hivyo, kifungo hicho kinatakiwa kuahirishwa baada ya wakili wa Kainth kukata rufaa kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, rufaa ambayo inampa nafasi ya kuchagua kulipa faini badala kifungo hicho.

Kwa mujibu wa sheria ya Hispania, watu waliohukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili wanaweza kuchagua kulipa faini ili wasitumikie kifungo hicho jela.

Sandro Rottman akiwa na Katie Price

Sandro Rottman akiwa na Katie Price

Kwa mujibu wa taarifa za kipelelezi zilizofikishwa mahakamani hapo, Rottman aliyekuwa na umri wa miaka 43 alifariki wakati anapatiwa matibabu hospitalini baada ya kushambuliwa na Kainth.

Ilielezwa kuwa Kainth alifika katika mgahwa huo kupata chakula akiwa na mwenzi wake na baadae walianzisha vurugu baada ya kubaini kuwa picha za binti wao zilikuwa kwenye iPad ya mtu huyo.

Harakati Za Kumsaka Bingwa Wa SDL Kuendelea Kesho
Waziri Mkuu Awafuta Kazi Vigogo Bandarini, Ni Baada Ya Kushtukiza Na Kukuta Madudu