Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Mulamu Ng’ambi ameeleza kinachoendelea kuhusu mazungumzo na Tume ya Ushindani( FCC ) juu ya mchakato wao wa mabadiliko ya kiuendeshaji wa klabu yao.

Mulam ametoamaelezo ya suala hilo alipohojiwa na kituo cha Radio cha East Africa kupitia kipindi cha Kipenga Extra, jana Jumanne (April 13).

Mulamu alisema: ”Hili jambo la FCC na Simba bado lipo kwenye majadiliano na mpaka sasa bado tupo kwenye mazungumzo ili kuweza kufika mwisho hizo mnazoziona ni vipande vipande tu vya taarifa hivyo pale itakapofikia mwisho tutalitolea taarifa.”

”Barua tunazozipata ni nyingi kutoka FCC, na hata leo pia, hatuwezi kuongea chochote kwakuwa hayo ni mawasiliano baina yetu na wao hivyo ikifika wakati wa kulileta kwa umma tutalileta kwa utaratibu.”

Kuhusu Mohamed Dewji kutweet kudai mchakato unatakiwa uanze upya, Mulamu Ng’ambi amesema: ”Nisingependa kujadili suala ambalo lipo katika mitandao ya kijamii kwa kuwa mtu anaweza kuposti chochote na inategemea ametafsiri kitu gani, hivyo tusubiri ikifika wakati tutaueleza umma”.

Mama wa kambo wa Obama afariki dunia
Azam FC yajizatiti kwa JKT Tanzania

Comments

comments