Mama wa Kambo wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, Kezia Aoko Obama amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Kifo chake kimethibitishwa na Mtoto wake Auma Obama kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo ameeleza kwa masikito kumpoteza mama yake.

Aidha wanafamilia wamesema kuwa Kezia amefariki akiwa anapokea matibabu hospitali nchini Marekani kwa muda mrefu.

Madereva bajaji, bodaboda walalamikia tabia za askari barabarani

Kezia alikuwa Mke wa kwanza wa baba yake aliyekuwa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.

Mazishi ya Kezia yanatarajiwa kufanyika leo Aprili 14, 2021 nchini Uingereza kwa kufuata taratibu za dini ya Kiislamu, hata hivyo familia yake inafikiria ni kwa namna gani wataweza kubeba mabaki ya marehemu na kuyapeleka Kenya.

Kifo cha Kezia kinakuja muda mfupi baada ya kifo cha bibi yake Barack Obama, Sarah Obama aliyefariki dunia mnamo Machi 29, 2021.

Biden kuondoa jeshi la Marekani Afghanistan
Mjumbe Simba SC afunguka mchakato wa mabadiliko