Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ ametimiza ahadi yake ya kuandaa Pambano la Kimataifa la Masumbwi, baada ya kutambulisha Mo Boxing.

Mo Dewji ambaye pia ni Rais wa Heshima na Mwekezaji Mwenza wa Klabu ya Simba SC alitangaza kuanzisha Mo Boxing mapema mwaka huu, kama sehemu ya kuendeleza michezo nchini Tanzania, baada ya kufanya hivyo upande wa Soka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kupitia ukurasa wa Mtandao wa Instagram wa Mo Dewji, Mo Boxing imeandaa Pambano la Bondia wa Tanzania Ibrahim Class dhidi ya Bondia kutoka nchini Mexico Alan Pina.

Pambano hilo limepangwa kuunguruma jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Next Door Arena, Septemba 30.

Taarifa hiyo imeeleza: @mo_boxing_tanzania inakuletea moja ya pambano KUBWA ZAIDI la mwaka likishirikisha mabondia kutoka #Tanzania, #Ghana, #Kenya, #UAE #Mexico. Akiongoza tukio kuu: Bondia kutoka Tanzania Ibrahim Class Vs. Alan Pina kutoka Mexico.


Wapi? Next Door Arena, Dar es Salaam
Lini? Septemba 30, 2022

Uuzaji wa tiketi utatangazwa hivi karibuni kwenye @otapptz
Asante kwa wadhamini wetu wakuu @boxertanzania na pia kwa @whitesands_resort @metlgroup (#MoXtra) @otappt

Sababu tatu zilizomng'oa Zoran Maki Simba SC
Taarifa binafsi za mitandao ya simu kulindwa