Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa timu ya Tanzania Prisons amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Februari kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2015/2015.

Mkopi katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, alicheza mechi zote nne za timu yake dhidi ya Mbeya City, Yanga, Mwadui na Mgambo Shooting. Alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika mechi hizo ambapo zote ilitoka sare, hivyo kupata jumla ya pointi nne.

Katika mechi hizo ambapo Tanzania Prisons ilifunga mabao matatu, Mkopi alifunga bao moja na kusaidia kupatikana mabao mengine mawili.

Mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa amefunga mabao sita kwenye Ligi hiyo, aling’ara zaidi katika mechi mbili kati ya hizo nne ambapo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Mkopi ambaye ni mshambuliaji wa kati alichaguliwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa mkoani Shinyanga, na ile dhidi ya Yanga iliyofanyika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa Februari, Mkopi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.

Wachezaji bora wa miezi miwili iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba 2015), na beki Shomari Kapombe wa Yanga (Januari 2016).

Mwamuzi Wa Kike wa 'Simba Na Yanga' Kuchezesha Kombe La Dunia
Wajumbe Wa TFF Kukutana Mwishoni Mwa Juma Hili