Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, ameendelea kuwatupia vijembe baadhi ya waandishi wa habari wanaoshinikiza afukuzwe kwazi kutokana mwenendo mbovu wa kikosi chake kwa msimu huu.

Mourinho, amewashukia baadhi ya waandishi wa habari kwa kuwaambai katu hawezi kung’oka Stamford Bridge kama wao watakavyo na badala yake ataendelea kuwepo klabuni hapo kama mkataba wake unavyoeleza.

Mwishoni mwa juma lililopita, Jose Mourinho alitoa maneno ya kushangaza mara baada ya mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Southampton, ambao waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Mourinho, alisema Chelsea hawawezi kumfuta kazi, na kama watafanya hivyo watakua wamemuondoa meneja aliye bora.

Mapema hii leo kituo cha televisheni cha Sky Sports, kimeripoti kwamba meneja huyo kutoka nchini Ureno, ameendelea na maneno ya shutuma kwa baadhi ya vyombo vya habari ambapo amekuja na suala jipya kwa kusema ataondoka Chelsea kama wachezaji wake watataka iwe hivyo.

Hata hivyo kauli hizo tata za Mourinho zinachukulia kama sehemu ya kujihami kwake dhidi ya mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovic, ambaye siku zote amekua hapendezwi na matokeo mabaya kikosini mwake.

Chelsea, wameendelea kusota katika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi ya nchini England kwa kumiliki point 8, walizozichuka katika michezo miwiwliw aliyoshinda na mingine miwili waliyotoka sare huku wakikubali kupoteza michezo minne hadi sasa.

Wenger Awachimba Mkwara Wachezaji Wake
Muasisi Mwingine Wa Tanu Na CCM Ahamia Chadema, Anamzidi Kingunge