Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), linafanya kazi kwa ushirikiano na mashirika dada likiwemo la Mpango wa Chakula Duniani, WFP na la Chakula na Kilimo, FAO kutekeleza mradi wa ‘Baho Neza’ (Ishi Vizuri’), kwa kutumia maafisa ustawi wa jamii wenyeji wanaojitolea.

Mashirika hayo matatu ya Umoja wa Mataifa, UNICEF, WFP na FAO, pia yanashirikiana na shirika la kimataifa la World Relief, tawi la Rwanda ili kuutekeleza mradi huo wa Baho Neza, kuleta mabadiliko chanya ya kijamii na kiuchumi katika maisha ya wakazi wa wilaya tano nchini Rwanda, ikiwa ni pamoja na Kirehe, Burera, Nyamagabe, Karongi, na Rutsiro.

Afisa ustawi wa jamii na mhamasisha maendeleo wa Wilaya ya Kihere Alphonsine Dorcelle amesema wanafanya kazi na wadau wengine ambao walichaguliwa katika vijiji vyote ili kuunda kundi kubwa litakalofanikisha mpango huo.

Nyumba bora za makazi nchini Rwanda.

Amesema, “Kupitia Mpango wa UN Moja, ambapo mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa hushirikiana kutekeleza miradi, nchini Rwanda, tunawatembelea hao wadau au washirika wetu ili kujadili shida zinazokabili kaya zao. Halafu lile tatizo tunalolikuta, tunalitafutia ufumbuzi.”

Kutokana na wengi kuguswa na matokeo ya mradi, wananchi hao wamesema mashirika hayo yamewasaidia kuleta mwamko katika maeneo yao na kwamba awali hatukuwa na bustani za mbogamboga na miradi mingine ambayo kwasasa inawasaidia kupata kipato.

Naye, Afisa ustawi wa Jamii, Jean de la Croix ambaye hujitolea katika mradi huo wa Baho Neza, ametoa ushuhuda wa namna mradi huu unavyowaletea mitazamo chanya kwa kudai kuwa, “niliitembelea nyumba ya mmoja wa wadau wetu nikakuta hawawezi kumudu kujenga choo lakini kwasasa mambo ni tofauti.

Rwanda

Mradi wa Baho neza ‘Ishi Vizuri’ umeandaliwa na Mashirika hayo ili kuziwezesha kaya masikini kuishi maisha bora kwa ujenzi wa nyumba bora, kilimo kikuu, ufugaji na ulimaji wa bustani za mbogamboga nyumbani, unaowasaidia kupata mboga na kipato cha kujikimu na maisha.

Polisi wabaini chanzo kikuu ajali za Barabarani
Uchaguzi Mkuu Kenya: Tuhuma za utata kwa IEBC