Kiongozi wa muda mrefu wa Zimbabwe, Rais Robert Mugabe amesema kuwa, hatomlazimisha mtu kumteua kuchukua nafasi yake endapo chama chake kitahisi anahitaji kustaafu bali itabidi chama chake  kiitishe mkutano mkuu kumchagua kiongozi mwingine.

Aidha, Mugabe ambaye ndiye kiongozi mzee kuliko wote duniani, alitimiza umri wa miaka 93 siku ya Jumanne na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980, hivyo kuitumikia Zimbabwe zaidi ya miaka 40, tangu nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1980.

Mugabe aliungwa mkono na maelfu ya wafuasi wake kusherekea siku ya kuzaliwa kwake katika shule ya Matobo nje kidogo ya mji wa pili kwa ukubwa wa Bulawayo. huku wanaharakati mbalimbali nchini humo wakilaani kutumika kwa gharama kubwa ya sherehe hiyo wakati nchi hiyo ikikabiliwa na hali mbaya ya uchumi.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwa muda wa saa moja kiongozi huyo  alimshukuru mwenyezi mungu kwa kumpa maisha marefu na muda mwingi kuzungumzia maisha yake mwenyewe.

Maalim Seif: Nitaunda Serikali isiyokuwa na Mawaziri Mizigo
Breaking: Bodaboda wamshambulia dereva daladala (Video)