Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikionesha orodha ya wabunge wanaolidai Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, wapo wabunge wanaoonekana wanalidai Bunge hilo, hatua ambayo Spika amesema imesababisha apigiwe simu na wengi waliowahi kuwa wabunge.

Ndugai ametoa ufafanuzi huo jana Bungeni, akieleza kuwa orodha inayosambaa ya madeni ni ya mwaka 2018 na kwamba kwa sasa hakuna anayelidai Bunge hilo.

“Kuna watu walipomaliza ubunge maisha yao ni magumu kweli, sasa anasikia kuwa anadai yaani ni tabu tupu, acheni, acheni jamani siyo kweli,” amesema Spika Ndugai.

Amesema Bunge hilo lililipa stahiki za wabunge wote waliomaliza muda wao. Hata hivyo, alimtaja mbunge aliyedai kuwa yuko ng’ambo ambaye alisema alipoingiziwa fedha zake zilichukuliwa zote kwakuwa alikuwa na madeni.

Baadhi ya watu wametafsiri kuwa aliyetajwa kuwa yuko ng’ambo ni aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye yuko wiki hii alikuwa nchini Kenya akizindua kitabu chake, lakini tangu mwaka 2017/18 alikuwa nchini Ubelgiji.

Covid 19: Museveni afuata nyayo za Magufuli
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 26, 2021