Video ya wimbo wa rapa Joh Makini ‘Nusu Nusu’ imezifunika video nyingi za Afrika kwenye Official Chart ya MTV Base na kukamata nafasi ya kwanza katika kituo hicho cha runinga cha kimataifa.

Video hiyo iliyofanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Justin Campus akishirikiana na Vanessa Mdee iliwashirikisha wasanii wengi wa Tanzania kama Jux, Sheta, G- Nako na Nahreel.

Joh anazidi kupanda ngazi na hivi sasa anapika collabo kubwa na rapa mwenye jina kubwa zaidi afrika kusini, AKA.

Lowasa: Anaesema Mimi Mla Rushwa Alete Ushahidi
Davido Na Diamond Kuperform Pamoja Kwenye Tuzo za MTV/MAMA 2015