Beki kutoka nchini Kenya Joash Onyango Achieng amesema wataendelea kupambana ili kuzuia kutokufungwa kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC leo inarejea kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza mchezo wa kiporo dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Beki huyo ambaye ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Didier Gomes, amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote na watapambana ili wasifungwe.

“Tumemaliza mashindano ya kimataifa hatua ya kwanza na tunaamini kuna hatua nyingine ambayo inakuja tupo tayari kwa ajili ya robo fainali na tutapambana ili tupate matokeo mazuri kwa kulinda lango ili tusifungwe.

“Kwenye ligi pia tunazidi kupambana ili kupata matokeo mazuri, kila kitu kinawezekana na tutazidi kushindana kila wakati,”  amesema Onyango ambaye kwenye ligi ametupia bao moja.

Simba SC inarejea kwenye Ligi Kuu huku wakiwa na moto wa mafanikio kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, ambapo wametinga hatua ya Robo Fainali, baada ya kuongoz amsimamo wa kundi A, lililokuwa na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita ya DR Congo na Al Merrikh ya Sudan.

Azam FC yajizatiti kwa JKT Tanzania
Harmonize acharuka kusambaa kwa video za utupu