Bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao anatarajiwa kurejea ulingoni baada ya kufanyiwa matibabu ya bega kikamilifu.

Awali alifanyiwa upasuaji baada ya kupoteza pambano dhidi ya Floyd Mayweather mapema mwezi May mwaka huu.

Bondia huyo alipanda ulingoni katika mchezo huo huku akiwa na majeraha ya bega, ambayo aliyapata wakati akiwa mazoezini.

Pacquiao, amefanyiwa vipimo vya mwisho vya MRI na amebainika yupo safi na ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kupambana ulingoni dhidi ya mpinzani yoyote atakayejitokeza kwa sasa.

Taarifa zinaeleza kwamba, Pacquiao huenda akapambana na bondia kutoka nchini England, Amir Khan.

Palikua na taarifa za kufanywa kwa mazungumzo baina ya viongozi wa mabondia hao mapema mwezi huu.

Carragher Amvisha Taji Daniel Sturridge
Jaji Lubuva Aonya Wanasiasa Wanaotumia Maneno Haya