Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajia kupambana ulingoni Agosti 27 mwaka huu na bingwa wa Masumbwi, Francis Cheka katika pambano lililolenga kuhamasisha usafi wa mazingira.

Taarifa ya pambano hilo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na bondia Cheka ambaye ameeleza kuwa kampuni yake ya Cheka promotion ndiyo iliyoandaa tukio hilo la uhamasishaji.

Cheka

Kupitia pambano hilo la ‘kimkakati’, Cheka amesema anaamini watakuwa wameunga mkono zoezi la uhamasishaji wa usafi lililotiliwa mkazo na Rais John Magufuli.

Akizungumzia pambano hilo, Cheka alisema kuwa huwa anaogopa mtu asiyejua ngumi anayekubali kupanda ulingoni na yeye.

“Siwezi kujua mkuu wa mkoa maandalizi yake ambayo amejiandaa lakini siku zote namuogopa mtu ambaye anaamua mapambano na mtu anayejua ngumi,” Cheka anakaririwa.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo, kampuni yake itaelekea mikoani pia kuhamasisha mabondia kushiriki katika zoezi la usafi.

Credit: Emmy Mwaipopo

Kevin Hart avuta Jiko
Video Mpya: AY - El Chapo