Siku kadhaa baada ya kukamatwa tena kwa mfabiashara maarufu wa dawa za kulevya kutoka Mexico, JoaquÍn “El Chapo” Guzmán, imedaiwa kuwa ‘mahaba niuwe’ ni moja kati ya vyanzo vilivyopelekea kukamatwa kwa bilionea huyo wa unga.

Maafisa wa Mexico walisema Jumanne wiki hii kuwa penzi la muigizaji maarufu wa Tamthilia nchini Mexico, Kate del Castillo ni moja kati ya vyanzo vilivyopelekea kukamatwa kwa bilionea huyo akiwa mafichoni.

Imeelezwa kuwa mrembo huyo aliyemvutia sana El Chapo alikuwa akiwasiliana naye mara kadhaa kwa jumbe tamu za mahaba ambazo zilichapishwa kwenye magazeti na Mamlaka za Mexico zilikiri kuwa ni jumbe za kweli za mawasiliano kati ya wawili hao.

Castillo anadaiwa kumkutanisha El Chapo na muigizaji maarufu, Sean Penn katika moja kati ya maficho yake na wawili hao walifanya mahojiano maalum Oktoba mwaka jana, ambayo Penn anayatumia kuandika simulizi la kweli la maisha ya El Chapo.

Castillo, enzi za ujana

Kate del Castillo, enzi za ujana

Sehemu ya jumbe za mawasiliano kati ya El Chapo na Castillo zilizonaswa zinaeleza:

“Good afternoon. How is the best woman in the world and the most intelligent, whom I admire very much?” aliandika El Chapo. Ujumbe mwingine ulionesha kuwa anamthamini sana mrembo huyo ulisomeka, “I’ll care for you more than my own eyes. You’re so beautiful, my friend, in every aspect”

Oktoba 29, El Chapo alienda mbali na kumueleza mrembo huyo kuwa anataka kumtambulisha rasmi kwa mama yake, “I must say, my mother wants to meet you. I told her about you.”

Mrembo huyo pia alimuandikia ujumbe unaoonesha kukubaliana na uwepo wa El Chapo katika maisha yake huku akieleza kuwa unamfanya ajisikie yuko salama zaidi.

“I must confess that I feel protected for the first time. You’ll know my story when we have time to speak, but for some reason I feel safe and I know you know who I am, not as an actress or a public figure, but as a woman, as a person,” del Castillo alimuandikia El Chapo.

Oktoba 10, alimtumia ujumbe mwingine akieleza jinsi alivyovutiwa na simulizi la El Chapo kiasi cha kumnyima usingizi, “I don’t sleep much since I saw you. I’m very excited about our story….It’s all I think about.”

Lakini pia, kama watu waliozama katika dimbwi la mapenzi, El Chapo alimtumia mrembo huyo zawadi kumpongeza katika siku yake ya kuzaliwa, zawadi ambayo ilimteka mrembo huyo aliyekuwa anatimiza miaka 43, Oktoba 25 mwaka jana.

“What a nice birthday gift! Thank you! We will hug very soon!” Ulisomeka ujumbe wa Castillo akimshukuru El Chapo.

Hata hivyo, jana (Januari 13), mrembo huyo alitumia mtandao wa Twitter kufikisha ujumbe kwa mashabiki wake akikosoa vyombo vy habari kwa namna vinavyoandika na kuripoti habari hiyo.

Mayanja Akosoa Mipango Ya Kocha Dylan Kerr
Zilizochukua Nafasi Magazeti Ya England Leo