Ikiwa imesalia siku moja Kikosi cha Simba kuvaana na Yanga, Jeshi Polisi Kanda Maalumu ya Dar, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kuimarisha ulinzi katika mchezo huo wa watani wa jadi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa, amesema: “Tumejipanga kuimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zinazoingia na kutoka uwanjani hapo kuhakikisha hakutokei vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani.”amesema Kamanda Mambosasa

“Tunatoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa soka kufika uwanjani mapema ili kuepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani hapo kwani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha,” amesema.

“Mashabiki waepuke kuingia na chupa za maji majukwaani, kuingia na silaha ya aina yoyote, kupaki magari ndani ya uwanja pasipokuwa na kibali maalum pamoja na kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziruhusu,” amesisitiza Kamanda Mambosasa.

Wakati huo huo Uongozi wa Yanga umeweka wazi kwamba nyota wao wawili wamerejea kikosini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba.

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa maandalizi pamoja na mipango inakwenda vizuri hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi kila kitu kitakuwa sawa.

“Wachezaji waliokuwa majeruhi tayari wamerejea.  Dickson Job pamoja na Abdalah Shaibu, ‘Ninja’ walikuwa na maumivu ila kwa sasa wanaendelea vizuri na wamerejea.

Mpaka sasa Simba ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wamejikusanyia alama 61, wakifuatiwa na Young Africans wenye alama 57, licha ya kwamba wamecheza michezo miwili zaidi ya Simba.

ICC yamhukumu Ongwen kifungo cha miaka 25 jela
Prof. Shemdoe atengua kitendawili cha uhamisho