Uongozi wa klabu bingwa nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain umesisitiza kuwa katika mipango ya kukamilisha azma ya kufanya kazi na meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger.

PSG kwa miaka kadhaa wamekua na lengo hilo, kutokana na kupendezwa na falsafa za ufundishaji za meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, ambaye amedumu kwa kipindi kirefu katika ligi ya nchini England akiwa na klabu ya Arsenal pekee.

Lengo kubwa la viongozi wa PSG ni kutaka kuona uwezo wa klabu hiyo unaendelea kubaki katika hali ya ushindani barani Ulaya, na wanaamini Wenger ni mmoja wa mameneja ambao wataweza kufikia lengo wanalo likusudia.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya PSG, umekua ukikutana na vikwazo mara kwa mara, pale wanapo jaribu kushawishi harakati za kumuajiri Arsene Wenger, kutokana na msimamo wa babu huyo ambaye ana uchu wa kutwaa ubingwa wa England akiwa na Arsenal.

Wenger ameonyesha msimamo wa kutokukubaliana na matakwa ya viongozi wa PSG kwa sasa, kutokana na kuamini wazi mchango wake bado unahitajika kwenye klabu ya Arsenal ambayo alianza kuinoa mwaka 1996.

Wenger amefikia hatua ya kusema hatokua tayari kufanya kazi na PSG katika kipindi hiki, kutokana kuheshimu mkataba wake ndani ya Arsenal, halia mbayo inaambatana na mapenzi ya dhati dhidi ya klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London.

Mwishoni mwa juma alipofanyiwa mahojiano na muandishi wa habari wa gazeti la L’Equipe la nchini Ufaransa, Wenger aliendelea kusisitiza kutokua taayari kuondoka Arsenal na kurejea nchini kwao Ufaransa kufanya kazi na PSG, labla ikitokea anatimuliwa kazi huko Emirates Stadium, atafikiria kufanya hivyo.

Mkataba wa sasa wa Arsene Wenger kwenye klabu ya Arsenal unatarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao wa ligi.

Saad Kawemba: Kipre Tchetche Hang’oki Azam FC
Steve McClaren Kuingia Vitani Na Slaven Bilic