Q-Chief au Q-Chillah anaamini kuwa muziki wake unathamani kubwa japo haupewi heshima inayostahili hivi sasa lakini utapata thamani zaidi atakapotangulia mbele za haki.

Msanii huyo ameiambia EATV Radio kuwa watoto wake watafaidi matunda ya muziki wake kutokana na uwezo wake wa kutunga na kuimba nyimbo zinazoishi muda mrefu zaidi.

“Mimi nimepiga muziki unaoishi kuliko maisha yangu. Hata nikifa leo thamani yangu itakuwa mara tatu zaidi ya nilivyo hai. Kwahiyo, muziki wangu unaweza hata ukawasomesha watoto wangu,” alisema Q- Chillah.

Aliongeza kuwa ubora wa nyimbo zake unawafanya wasanii wengine kumfuata na kumuoma wazifanyie remix.

“Lakini naangalia, anaenda kui-waste au anaenda kuitengeneza?” alisema.

Ulimwengu, Samatta Watua Japan
Kendrick Lamar Afunika Tuzo Za Grammy 2016, Aongoza Kutajwa