Katika hali ya kushangaza, Rais wa nchi ya Mauritania ameingilia kati mechi ya fainali ya Super Cup na kuamuru timu zipigiane penati ili kupata bingwa huku zikiwa zimesalia dakika 27 kabla mchezo kumalizika.

Kwa mujibu wa sheria na kanuni za mashindano husika ya mpira wa miguu, mchezo wowote wa fainali huamriwa kuingia kwenye hatua ya penati tano tano mara baada ya kuchezwa kwa dakika 120 bila kupata mshindi.

Mtu pekee mwenye uwezo wa kutoa maamuzi hayo ni refarii wa mchezo.

Lakini Rais huyo Mohamed Ould Abdel Aziz hakujali hilo na badala yake alitumia mamlaka yake kama mkuu wa nchi na kuamuru mchezo umalizike kwa mikwaju ya penati mara moja licha ya dakika za mchezo kutofika mwisho.

Inaelezwa kuwa Rais huyo alikerwa na jinsi mechi hiyo ilivyopooza ambayo ilihusisha timu ya FC Tevregh Zeina dhidi ya ACS Ksar na ndipo ilipotimia dakika ya 63 ya mchezo, akaamuru zipigwe penati ili atoke uwanjani akafanye shughuli zingine.

Wakati penati hizo zinaamriwa kupigwa timu zote zilikuwa zimefungana bao 1-1, na hadi mikwaju ya penati inakamilika, Zeina ilichomoza na ubingwa na kukabidhiwa kombe.

Man City Waendelea Kujitanua Kwa Kutunisha Mfuko
Jipange: Kutupa Taka Hovyo faini 50,000, Watakaosaidia Kukamata Kuzawadiwa