Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, leo tarehe 1 novemba 2016,  wamezindua barabara ya mchepuko Southern Bypass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiiji la Nairobi, sherehe ya  uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 28 inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Magufuli  amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo itawasaidia wananchi wa kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla,pia ameishukuru  serikali ya china na benki yake  ambayo imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo. ”Wanananchi wanataka maendeleo na maendeleo  ndio haya,barabara hii itasaidia kuinua uchumi na mambo ya kijamii” alisema Magufuli.

Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta  amesema kujengwa kwa barabara hiyo  kumesaidia kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Nairobi, pia amemshukuru rais Magufuli kwa kuungana nae katika uzinduzi huo na kuongeza kuwa ufunguzi wa barabara hiyo utaongeza  utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara zinazounganisha Tanzania na Kenya.

Kabla ya uzinduzi huo Rais Magufuli alitembelea kiwanda kidogo cha kusindika maziwa cha Eldoville kilichopo katika eneo la Karen ambacho kinamilikiwa na familia ya mkulima. Kiwanda hicho kilianza kwa kuzalisha chini ya lita 1,000, lakini kwa sasa kinazalisha lita 5000 kwa siku hadi kufikia lita 70,000 kwa mwaka.

Wakala wa majengo Tanzania waanza kutimiza ahadi za Rais Magufuli
Raundi Ya 14 Ligi Kuu Soka Tanzania Bara