Rais wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona, Josep Maria Bartomeu amejibu tetesi zilizochukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari kuhusu mipango ya klabu ya Man Utd ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Neymar da Silva Santos Júnior.

Bartomeu amesema taarifa hizo amezipokea kwa mikono miwili na zimemfurahisha kutokana na dau kubwa la paund million 240 lililotajwa.

Rais huyo aliyeingia madarakani mwezi uliopita amesisitiza kwamba ni wazi ubora wa mshambuliaji huyo anapokua uwanjani ndio umesababisha kutajwa kwa dau kubwa kama hilo ambalo litavunja rekodi ya dunia katika usajili.

Hata hivyo Bartomeu amesema pamoja na kufurahishwa huko, FC Barcelona hawana mpango wa kumuachia mshambuliaji huyo kuondoka katika kipindi hiki na badala yake wanafikiria kumuongeza mkataba mpya.

Mkataba wa sasa wa Neymar Junior, ambao aliusaini wakati akijiunga na FC Barcelona mwaka 2013 akitokea nchini kwao Brazil kwenye klabu ya Santos, unatarajiwa kumalizika mwaka 2019.

Pamoja na tetesi hizo kujibiwa, uongozi wa Man Utd haujasema lolote mpaka dakika hii, kuhusu ukweli wa jambo hilo ambalo lilichukua nafasi kubwa katika vichwa vya habari duniani.

Neymar amekua msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya FC Barcelona akishirikiana na Lionel Messi pamoja na Luis Suarez na tangu alipotua Camp Nou ameshafanikiwa kufunga mabao 31 katika michezo 59 aliyocheza.

Mrembo Wa Miaka 16 Akiri Kuwa Gaidi, Amiliki Mabomu
Video: Kardashians waizimia ‘Ojuelegba’ ya Wizkid