Beki wa Real Madrid Sergio Ramos amesema hakuwahi kutaka kuondoka Bernabeu, licha ya taarifa kadhaa kumhusisha na kuhamia Manchester United.

Ramos, ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano amesema,

“Wazo langu lilikuwa kubakia hapa na kustaafu hapa kama rais angeruhusu hilo, na na ninashukuru sasa nina changamoto mpya ya kuwa nahodha wa timu hii.

“Sikuwahi kusema nataka kuondoka, nilikuwa kimya. Sikusema chochote kutokana na kuheshimu wachezaji wenzangu na rais, sikuwahi kupiga simu kwenye ofisi yetu na kutaka fedha zaidi.”

Azam FC Kurejea Dar Leo
Lowassa: Nitakomesha Wizi Wa Kura, Nchi Itaenda Spidi