Mwananmuziki maarufu duniani wa muziki wa Pop kutoka nchini Marekani, Ariana Grande ameolewa na mchumba wake Dalton Gomez kwa harusi ‘ndogo ya faragha’.

Kwa mujibu wa shirika la Habari la PA, Grande mwenye umri wa miaka 27 amefunga ndoa mbele ya watu wasiopungua 20 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Itakumbukwa Disemba 2020 Grande alitagaza kuwa alivishwa pete ya Uchumba na Gomez, ambaye ni wakala wa mali isiyohamishika wa Los Angeles mwenye umri wa miaka 25.

Grande na Dalton Gomez walifunga ndoa na kukamilisha Harusi yao iliyofanyika nyumbani kwake California, kwa mujibu wa ripoti.

Mambosasa aondolewa Dar es Salaam
India: Maambukizi Covid-19 yapindukia Mil. 25