Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel ametoa siku saba kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Mkoa huo kuwasilisha kwenye vyombo vya dola majina ya wakusanya mapato ya Halmashauri ya Sengerema waliohusika na upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 350 ili wachukuliwe hatua za kisheria

Ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kujadili utekekezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuishia Juni 30, 2020.

Amesema kuwa kipindi hicho Halmashauri ya Sengerema ilipata hati yenye mashaka hali iliyomlazimu kutoa agizo la kukamatwa kwa wakusanya mapato hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga ameahidi kutoa ushirikiano katika kuwabaini waliohusika na upotevu wa fedha hizo, kwani wengi wao ni watumishi wa umma na majina yao tayari wanayo.

Ambundo anukia Jangwani
Meneja Simba SC afichua siri