Mama mtoto wa Rick Ross, Tia Kemp amemfungulia mashitaka kiongozi huyo wa MMG akidai kuongezwa kiasi cha fedha ya matunzo ya mtoto wao, William Roberts III.

Kwa mujibu wa TMZ, Tia anaiomba mahakama aongezewe kiasi cha fedha ya matunzo kutoka $1,951 kwa mwezi hadi $2,800 kwa mwezi.

Tia anadai ongezeko hilo kwa kuwa amebaini ongezeko la mali za rapper huyo akitaja majumba ya kifahari yaliyoko Atlanta na Miami.

Jumba liliko Atlanta lina thamani ya dola milioni 5.9 na lile la Miami lina thamani ya dola milioni 5.1.

Tia amedai kuwa mtoto wao anahitaji kiasi cha fedha cha ziada kumuwezesha kulipia mafunzo ya martia arts kwa sababu ana kipaji hicho.

Ray C Aweka Wazi Hisia Zake Kwa Rais Kenyatta, ‘Huwa Namuota ’
Picha: Kim Kardashian Azitosa Make Up Kwenye Jarida La Vogue