Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ ameendelea kuwa kimya kuhusu kikosi cha klabu hiyo ya Msimbazi.

‘Robertinho’ alitambulishwa rasmi kuwa Kocha Mkuu Simba SC Jumanne (Januari 03), na moja kwa moja alielekea Zanzibar kuitazama timu yake ikishiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amerejea jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Januari 06) na kukataa katakata kuzungumza kuhusu Simba SC, baada ya kuulizwa na Waandishi wa Habari ambao walitamani kusikia lolote kutoka kwake.

‘Robertinho’ amesema bado ni mapema mno kuzunguza kuhusu Simba SC, kwani anaamini muda upo mwingi na ipo siku atasema lolote kuhusu kikosi chake.

“Siwezi kuzungumza lolote kuhusu Simba SC, bado muda upo, ipo siku nitaongea.” amesema Kocha Robertinho

Kabla ya kujiunga na Simba SC Robertinho alikua akikinoa kikosi cha Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC, akikiongoza katika michezo 57, akishinda 43, Sare 9 na Kufungwa 6.

Mafanikio: Ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uganda na Kombe la Shirikisho nchini Uganda (2021/22), huku akitajwa kuwa Kocha Bora nchini humo msimu uliopita 2021/22.

Pia amekuwa Kocha wa kwanza kuifikisha Vipers SC hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kocha Mgunda ajibu tuhuma nzito Dar es salaam
Gianluca Vialli ameumaliza MWENDO