Aliyekua beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Brazil, Roberto Carlos amepuuzia taarifa zinazodai kuwa nyota wa Barcelona, Neymar anaweza kuhamia kwa mahasimu wao, Real Madrid.

Beki huyo wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil alisema kwamba anaweza kumhamisha Neymar kutoka Barcelona kwenda Real Madrid endapo atapewa jukumu la kuinoa klabu hiyo.

Jumapili Neymar alikuwa kwenye ubora wake tena akiwa na Barcelona  baada ya kufunga bao moja kati ya sita ambayo timu yake iliibuka na ushindi huo mnono dhidi ya Athletic Bilbao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.

Hata hivyo, pamoja na ubora huo Carlos anapotezea kama kunaweza kukawepo na uwezekano kwa nyota huyo akaitema Barcelona na kujiunga na Madrid.

“Haiwezekani nimewahi kusema hivyo siku za nyuma na watu wamekuwa wakilichukulia jambo hilo kwa umakini kwa sababu Real Madrid huwa inasajili wachezaji bora duniani,” alisema Mbrazil huyo ambaye amerejea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Hispania akiwa na timu yake ya zamani kwa ajili ya maandalizi ya kujiendeleza na kibarua chake cha ukocha.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia alisema kuwa ingekuwa jambo jema kama angeweza kufanya kazi chini ya kocha mpya wa klabu hiyo, Zinedine Zidane, lakini akasema kuwa dhamira yake kwa sasa ni kuendelea na mafunzo yake ya ukocha.

“Ningefurahi kama kungekuwepo na uwezekano huo lakini nipo mahali hapa kwa ajili ya mazoezi na kujifunza,” alisema Carlos na kuongeza kuwa kwa sasa ameanza mafunzo yake ya ngazi ya juu baada ya kutumia muda wa miaka mitano akifanya hivyo katika nchi za Uturuki, Urusi na India huku akisema ameshajifunza mengi lakini anaomba apewe muda.

 

Pinda awatahadharisha wabunge wa CCM
Man City Kuikosa Huduma Ya Pablo Zabaleta