Ukiwa umebaki takribani mwezi mmoja wawakilishi wa wananchi kukutana jijini Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu wa zamani, Mizengo Pinda amewatahadharisha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujipanga.

Akiongea hivi karibuni katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, Pinda alieleza kuwa kuongezeka kwa idadi ya wapinzani bungeni kutaleta ushindani mkubwa wa hoja ambapo kila upande utataka kufanya utafiti ili kujenga hoja nzito zaidi ya upande mwingine.

“Kuongezeka kwa idadi ya wapinzani kwa maana ya bunge, kitakachojitokeza pale ni kwamba inabidi kila upande ujiandae vizuri tutakapokuwa tunajenga hoja pale bungeni. Kwa hiyo kila upande utataka kufanya vizuri zaidi na kufanya utafiti zaidi. Lazima kila upande ujiandae sasa kwamba ukienda pale huna hoja ujue sasa kwamba nguvu ziko kila upande. Ukilegeza kamba utakuwa defeated,” alisema.

“Mimi naamini kabisa kwamba wapinzani wameongezeka kwahiyo watakuwa wameongeza nguvu ya ku-argue hoja zao pale bungeni, lakini naamini kwamba upande wa CCM kwa kuwa bado ni majority na wao sasa itabidi wajipange vizuri ili kuhakikisha kwamba wakifika pale wafanye utafiti wa kutosha na kujenga hoja vizuri na waonekane kwamba kweli wanatekeleza kile ambacho umma ulikuwa unatarajia,” aliongeza.

Hata hivyo, Pinda aliwataka wabunge wa pande zote kuhakikisha kuwa hoja na ushindani kati yao uwe kwa ajili ya manufaa ya umma na sio vingine.

 

Davido avunja rekodi hii kwa mamilioni ya Sony Music Global
Roberto Carlos Amkataa Neymar Real Madrid