Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameondoka hii leo kwenda Lubumbashi, Jamhuri ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kujiunga na klabu yake, TP Mazembe wakati sakata la uhamisho wake likiendelea.

Samatta anaondoka na Maofisa wa Wizara ya Michezo walioteuliwa kwenda kuzungumza na Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi kumshawishi amruhusu mchezaji huyo kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji.

Iwapo Katumbi ataendelea kusistiza msimamo wake wa kutaka Samatta aende Nantes ya Ufaransa, basi mchezaji huyo ataamua kubaki Mazembe amalizie miezi yake mitatu ya Mkataba wake ili aondoke kama mchezaji huru Aprili.

Serikali yakanusha uzushi uliosambaa kuhusu Rais Magufuli
Mkwasa Ashangazwa Na Maamuzi Ya Nadir Haroub Cannavaro