Serikali inanatarajia kuja na mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi 119 bilioni ambao utakaohudumia vijiji 34 vya Wilaya ya Ruangwa na 21 vya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hii leo Machi 31, 2023 wakati akizungumza na wakazi wa Ruangwa waliohudhuria hafla ya kutambulisha mafanikio ya miaka miwili ya Serikali iliyofanyika kwenye Ghala la Lipande, Wilayani humo.

Amesema, “mradi huu ambao utaanzia Nyangao, kuja Nanganga hadi Ruangwa kisha utaenda Chiola hadi Nachingwea. Mkandarasi ameshapatikana na mkataba umeshasaIniwa. Kwa hiyo mradi utaanza wakati wowoted hamira ya Rais wetu ni kuongeza uwezo wa upatikanaji wa maji kwenye miji yetu na vijiji vinavyozunguka miji hiyo.”

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta za elimu, afya, maji, barabara, madini na michezo ambapo kuhusu elimu kwenye Wilaya hiyo, amesema miundombinu imeboreshwa kwa kujenga shule mpya za Sekondari na za Msingi, ufundishaji kuimarika na ufaulu kuongezeka hadi asilimia 98. 

Aidha ameongeza kuwa, Wilayani humo kuna baadhi ya kata ambazo zina shule za sekondari mbili ambapo kata ya Likunja ina sekondari za Likunja na Kitandi na kudai kuwa, “kata nyingine ni Narungombe kuna ambako kuna sekondari za Liugulu na Narungombe ambapo Liugulu tumeamua iwe ni maalumu kwa wasichana na Narungombe iwe maalumu kwa wavulana.”

Odds kubwa Wikiendi hii, Bayern vs Dortmund, Man City vs Liverpool  
Ndalichako akagua maandalizi uzinduzi mbio za Mwenge 2023