Serikali imeshauriwa kuunda timu ya wataalamu na wafanyabiashara mashuhuri akiwemo Mohammed Dewji (Mo), ili kushauri na kutengeneza mazingira yatakayowafanya wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.

Ushauri huo umetolewa leo Aprili 9, 2021 bungeni na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 – 2025/26.

“Kuna jambo linanitia moyo lakini linanisononesha, tuna watu wazuri sana katika nchi hii katika mawazo mema ya kufanya biashara na hapa nimpongeze mpinzani wangu Mohammed Dewji ambaye tumesikia ameteuliwa na Rais wa Afrika Kusini kuwa ni mmoja kati ya watu watakao mshauri, sasa kama nchi tuna mtu kama yule mzuri wenzetu wamemuona sisi kama nchi tunamtumiaje?, ndipo napendekeza Serikali iunde timu ya wataalamu na wafanyabiashara mashuhuri watushauri tufanyeje kwenye masuala ya uwekezaji nchini,” amesema Tarimba.

Tarimba pia ametumia fursa hiyo kumpongeza Dewji kwa kuteuliwa kwake kuwa miongoni mwa watu wanaomshauri Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kwenye masuala ya uwekezaji nchini humo.

Mume wa Malkia Elizabeth, Prince Philip afariki
Serikali ikakope nje - Kimei