Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kimewasili salama mjini Unguja Kisiwani Zanzibar, tayari kwa Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2022 iliyoanza rasmi jana Jumapili (Januari 02).

Simba SC iliyoondoka Dar es salaam majira ya asubuhi, itaanza mchakato wa kulisaka taji la Mapinduzi 2022, keshokutwa Jumatano (Januari 05), kwa kucheza dhidi ya Selem View Uwanja wa Aman.

Simba SC imeelekea Zanzibar ikiwa na kikosi chake kamili, huku Kiungo Mshambuliaji kutoka Malawi Peter Banda akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa The Flames inayojiandaa na Fainali za Mataifa ya Afrika 2022 zitakazounguruma nchini Cameroon kuanzia mwishoni mwa juma hili (Januari 09).

Ahmed Ally akalia kiti cha Manara Simba SC

Mwaka 2021 Simba SC ilifika Fainali ya Kombe la Mapinduzi na kupoteza kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati dhidi ya Young Africans.

Ahemd Ally: Ni uzito wa dunia nzima
Al Shabab waua watu sita nchini Kenya