Simba imemsajili beki wa African Sports ya Yanga ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.

 

Taarifa zinaeleza beki huyo wa kati tayari ameishatua mjini Zanzibar na kujiunga na wenzake.

“Kweli Simba imemsajili beki huyo kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, ameungana na wenzake Zanzibar na ameanza mazoezi,” kilieleza chanzo.

Simba iko mjini Zanzibar ambako imeweka kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara ambayo tayari imeanza.

Simba imecheza mechi 9 tayari, iko katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 21.

Kinda La Kiafrika Lawanyima Usingizi FC Barcelona
Friends Rangers Yasajili Wanne Dirisha Dogo