Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku nne katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe, timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, kesho ijumaaa itacheza mchezo wa kirafiki wa mazoezi katika uwanja wa kwanza wa hoteli ya Kartepe.

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya ratiba ya Stars ambapo mchezo kocha wake atatumia kutazama maendeleo ya kikosi chake, kabla ya kurejea nyumbani tayari kupambana na Nigeria Septemba 05, mwaka huu katika mchezo wa kuwania kufuza kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017.

 

Timu imeendelea na mazoezi leo mara moja baada ya kufanya mazoezi mfululizo asubuhi na jioni kwa siku tatu, ambapo leo wamefanya mepesi kujiandaa na mchezo huo dhidi y timu ya Taifa ya Libya inayonolewa na kocha Javier Clemence raia na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania, Atletico Madrid, Atletico Bilbao.

Akiongelea maendeleo ya kambi nchini Uturuki, kocha mkuu wa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wanaendelea vizuri na progam yao ya mazoezi, ambapo wachezaji wote wanafanya mazoezi kwa usikivu na umakini mkubwa kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.

“Wachezaji wote wapo katika hali nzuri kama unavyoona, wanajituma, wanafanya mazoezi kwa nguvu, na kutokana na kuwa mazingira mzuri ya kambi, kila moja anaonyesha uwezo binfasi wa kutaka kupata namba katika kikosi cha kwanza” alisema Mkwasa.

Stars itacheza na Libya mchezo huo majira ya saa 5 kamili asubuhi kwa saa za Uturuki katika uwanja wa kwanza wa hoteli Kartepe, mudaa huo umepangwa na wenyeji kutokana na hali ya hewa itakayokuwepo siku ya ijumaaa.

Abdi Banda ni mchezaji pekee aliye majeruhi kwa sasa katika wachezaji waliopo kambini nchini Uturuki kufutaia kupata tatizo la kuchanika nyama za paja, na kwa mujibu wa daktari wa timu Dr, Yomba anapaswa kupumzika kwa takribani siku 10 kabla ya kuanza mazoezi mepesi tena.

Fabio Coentrao Atolewa kwa Mkopo AS Monaco
Bondia Wa Kike Anaetamba Kumpiga Mayweather Amchokoza Na Pesa