Mkurugenzi wa Uwekezaji na Utawala wa Kampuni ya michezo ya kubahatisha nchini Sports Pesa, Abbas Tarimba ameishauri klabu ya Young Africans kujifunza kutoka kwa Simba SC kutokana na ubora walionao kuanzia kwenye uwekezaji mpaka uwanjani.

Tarimba ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Dar es salaam ametoa ushauri huo kwa Young Africans akiwa bungeni mjini Dodoma, ambapo amesema mafaniko ya Simba SC yanaendelea kumpa nafasi ya kuamini soka la Tanzania lina nafasi kubwa ya kubadilika kuanzia sasa.

“Siku zote mimi nakuwa mkweli nimesema hata bungeni wakati wote Simba wakifanya vizuri mimi nawapongeza na walipofika si mzaha na wameinyanyua Tanzania na ninaiona Simba SC fainali itakuwa ni heshima kwa Tanzania na waliowekeza pale”

“Klabu zingine ziige mfano wa Simba SC na nimekuwa nikimpongeza pia Mwekezaji Mohamed Dewji kwa uwekezaji wake ambao umelipa na pia najua akina Mo Dewji wapo wengi Tanzania ni wakati sasa kutumia watu kama hawa kwa faida ya nchi” amesema Tarimba

Simba SC imetinga hatua ya Robo Fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya kuongoza msimamo wa Kundi A, lililokuwa na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita Club ya DR Congo pamoja na Al Merrikh ya Sudan.

Kwa sasa Mabingwa hao wa Tanzania Bara, wanasuburi Droo ya Robo Fainali na huenda wakapangwa na klabu za Kaizer Chief kutoka Afrika kusini ama klabu kutoka nchini Algeria MC Algiers na RC Belouizdad.

Harmonize acharuka kusambaa kwa video za utupu
Fraga atuma ujumbe Simba SC