Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo ametoa wito kwa Shirika la Viwango Tanzania TBS kuweka mpango maalum utakaosaidia wajasiriamali ambao wanafanya ujasiriamali mdogo ili kuweza kuwainua kupata viwango vya ubora.

Ameyasema hay leo Novemba 15, 2021wakati akizindua tuzo za ubora kitaifa kwa mwaka 2021/2022 katika ofisi za TBS makao makuu Jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania ni moja ya nchi wanachama iliyoitikia wito wa kuanzisha mashindano ya kitaifa mwaka 2020.

“Kwaweli kwa Tanzania tunapozungumza ujasiriamali mdogo , mkubwa na wakati tunazungumzia kundi kubwa zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wetu wapo katika maeneo hayo kwaiyo tungetaka kuona TBS inawapa uzito wa kutosha,” Amesema Waziri Mkumbo.

Aidha tuzo zimegawanyika katika makundi matano ikiwemo kundi la kwanza ni kampuni bora ya mwaka katika ukanda wa Afrika Kusini, bidhaa bora ya mwaka, huduma bora ya mwaka, muuzaji bora wa bidhaa nje ya nchi na tuzo binafsi ya mtu aliyechangia sana katika ubora.

Sambamba na hayo Waziri Mkumbo amewataka Wizara kwa kushirikiana na TBS kuhamasisha ushiriki katika mashindano ya mwaka huu ili waweze kushiriki kwa wingi zaidi.

Naye Mkurugenzi wa TBS Dkt Athuman Ngenya amesema kuwa TBS inaendelea kutoa elimu hasa kwa kundi la wajasiriamali wadogo ili waeze kushiriki kwa wingi zaidi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 16, 2021
Majaliwa atoa siku 3 kwa wasimamizi wa Mto Ruvu utatuzi changamoto