Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi.

Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Amesema sheria inairuhusu TRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye ana deni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.

Aidha amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa wa mwisho kabisa baada ya njia zingine zote za majadiliano kushindikana.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 22, 2021
Nyalandu awajibu waliojichanganya, awakaanga CHADEMA