Leicester City ndio mabingwa wa EPL msimu uliopita. Baada ya kuchukua ubingwa, mwenyekiti wa club hiyo Vichai Srivaddhanaprabha aliahidi kununua gari kwa kila mchezaji wa timu hiyo kama zawadi kutokana na mafanikio yao ya kuipa ubingwa timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe. Jana wakati wanaenda mazoezini kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa leo wa Ngao ya jamii dhidi ya Manchester United, wachezaji wengi walionekana na ndinga zao mpya aina ya BMW zenye thamani ya paundi 105,000 walizopewa na baada ya bosi wao kutimiza ahadi yake licha ya baddgi yao kutumia magari yao waliyonunua wenyewe.

Lissu asimulia machungu aliyoyaonja Rumande
Manji Awavua Uanachama Wajumbe Watatu Yanga