Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA limetangaza mabadiliko ya sheria ya mabadiliko ya wachezaji kuelekea fainali zamataifa ya Ulaya ‘UEFA EURO 2020’ zitakazofanyika msimu wa majira ya kiangazi (11 Juni 11 –Julai 11).

Sheria hiyo mpya itaziwezesha timu shiriki kufanya mabadiliko ya wachezaji watano katika mchezo mmoja, ambapo UEFA wamechukua sheria hiyo baada ya FIFA kuongeza matumizi ya wachezaji watano wanaotokea benchi katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, ambazo zitaendelea hadi Machi 2022.

Mabadilio hayo pia yatatumika kwenye michuano ya UEFA Nations League itakayoanza Oktoba na playoff ya kujikwamua kushuka daraja mwakani mwezi Machi pia zitaruhusu nafasi tano za mabadiliko kwa wachezaji wa timu zote shiriki. UEFA imesistiza sheria hiyo bado ni “halali” kwa michezo iliyoathiriwa na janga la Corona.

Uamuzi wa awali wa kuongeza idadi ya mabadiliko ya wachezaji kutoka watatu hadi watano ulifanywa wakati wa kwanza wa Janga la Corona ili kulinda wachezaji kutokana na majeraha yanayoweza kutokea wakati mchezo.

Kamati hiyo ya UEFA pia ilifanya uamuzi kuhusu kuingia kwa watazamaji kwenye mechi za UEFA. Iliamua kuwa watazamaji wataingia kwa asilimia 30 ya uwezo wa Uwanja, Lakini ikisema kwamba uamuzi juu ya idadi ya watazamaji wataoruhusiwa inapaswa kuwa chini ya Uamuzi wa mamlaka husika za mitaa / kitaifa.

Hii ni sheria ambayo imekuwa ikipitishwa sana katika ligi mbalimbali ulimwenguni, na Premier League ndiyo ligi pekee ya kubwa huko Ulaya ambayo haikuruhusu msimu wa 2020-21.

Msuva atangaza njaa Afrika
Facebook yapiga marufuku sauti ya Trump